Wednesday, September 19, 2007

hii ndiyo Klabu ya Juventus






Juventus Fooball Club

'Bibi Kizee cha Turin ndani ya Miaka 100 ya Soka'

Ni siku nyingine tena tunapokutana katika mfululizo wa kuchambua kwa undani historia ya klabu kubwa duniani, ambapo leo hii tupo nchini Italia tena baada ya kuwa nchini humo kwenye Klabu ya AC. Milan leo tunabaki huko huko lakini safari hii tukitua kwenye mji wa Turin, ambapo ndio makao makuu ya Klabu ya Juventus Football Club ambao wengine huiita 'Bibi Kizee cha Turin'. Hii ni kutokana na maombi ya wasomeji wengi kuomba kudadavuliwa klabu hii ambayo ni moja ya klabu kubwa duniani.



Juventus Football Club, ilianzishwa mnano Novemba 1 mwaka 1897, na kikundi cha Wasichana kutoka shule ya sanaa za majukwaani ya mji wa Turin nchini Italia iitwayo 'Massimo D'Azeglio Lyceum'. Waanzilishi wote walikuwa ni Wasichana wenye umri wa miaka kati 14 na 17 huku chanzo cha kuanzishwa kwake ikiwa ni eneo la Corso Re Umberto ambalo walikuwa wakilitumia wakati wa mapumziko.

Baada ya kuanzishwa jukudi za kuitangaza Klabu zilianza na katika kipindi hicho magazeti yanayoandika habari za michezo nchini Italia yalikuwa hayaipi nafasi kutokana na uchanga wake lakini hujudi ziliendelea kwa kasi na katika kipindi hicho mmoja ya waanzilishi wa Enrico Canfari aliandika waraka uliokuwa unaelezea juu ya kuzaliwa na madhumuni ya Klabu hiyoi ambayo kwanza ilikuwa changa ilikilinganishwa na klabu nyingine.



Lakini pamoja na juhudi hizo za kuitangaza lakini kulizuka mjadala mwingine jina halisi ya klabu ambapo kulipigwa kura kwa huku katika kinyang'anyiro hicho kukiwa na majina matatu yaliyoipendekezwa ambayo ni Società Via Fori, Società Sportiva Massimo D' Azeglio na Sport Club Juventus jina ambalo lilipitishwa kutumika rasmi.


Katika uchaguzi huo wa jina la Klabu pia ilihusiha baadhi ya Wanaume wachache walioonekana walikuwa na upeo wa kufanya mabadiliko na mwelekeo wa mbele zaidi.
Juventus ilianzishwa ikiwa na waasisi 13, ambao ni Gioacchino Armano, Alfredo Armano, Enrico Canfari, Eugenio Canfari, Francesco Daprà, Domenico Donna, Carlo Ferrero na Luigi Forlano.

Wengine ni Luigi Gibezzi, Umberto Malvano, Enrico Piero Molinatti, Umberto Savoia na Vittorio Varetti.
Rais wa kwanza wa Juventus, alikuwa Eugenio Canfari ambaye ni Kaka wa Enrico Canfari, (mmoja ya waasisi wa Klabu). Eugenio Canfari alikuwa ni mchezaji wa zamani wa timu ya Piazza D'Armi iliyokuwa na maskani yake kwenye kitongoji cha Crocetta katika mji wa Turin.

Kutokana na sababu mbali mbali Juventus ilifanya mabadiliko ya jina la Klabu kutoka Football Club Juventus na kuitwa Juventus Football Club na hii ilikuwa ni mwaka 1899, huku ikitumia rangi ya Pinki na Nyeusi kama rangi rasmi ambayo ilikuwa inajulikana nchini Italia kama Rosanero.

Juventus iliingia rasmi katika ligi kuu nchini Italia na tangu msimu wa mwaka 1900 huku mchezo wa kwanza katika michuano ya Klabu bingwa ilikuwa ni May 11 mwaka 1900 ilionesha uwezo mkubwa kwa kufanikiwa kutoa upinzani wa hali ya juu ambao wengi whawakuutarajia hasa baada ya kuibomoa timu ya FBC Torinese kwa bao 1-0 ambao ulisukumizwa Piazza D'Armi.

Msimu iliofuatia Juventus iliendelea kufanya vizuri baada ya kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano ya ligi kuu Serie A kwa msimu huo kwa kuisasambua timu ya Ginnastica Torino kwa bao 5-0 kisha kukutana na Milan Cricket na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 2-3.


Kutokana na kukua kwa soka la nchini Italia klabu hiyo ilianza mikakati ya kujiimarisha na kujipanua zaidi kwa lengo la kuwa timu bora na yenye uwezo mkubwa wa kufanya ushindani hivyo mwaka 1903 iliangaza macho sehemu mbali mbali barani Ulaya na kutua nchini England kwa kumsajili mchezaji John Savage kutoka Klabu ya Nottingham.

Juventus iliendelea kuwa Klabu kubwa na wenye kutishia Klabu nyingine barani Ulaya kwa kufanya usajili imara na makini uliofanikiwasha timu hiyo kuwa bora ndani na nje ya Italia ikiwa chini ya Rais Alfredo Dick ambaye baadaye aliondoka na kuiacha ikiwa imara pengine kuliko kipindi kingine chochote kile.



Tangu Januari 13 mwaka 1907 hadi kufikia wakati wa vita Kuu ya kwanza ya Dunia mwaka 1914 soka la Italia ilimilikiwa na Klabu nyingine baada ya Juventus kuanza kupoteza umaarufu huku baadhi ya Klabu zilizokuwa tishio kama Piedmont club Pro Vercelli na Casale zikiendelea kuwa juu lakini zilikabiliwa na tatizo kubwa ambalo ni kusekana kwa michuano mikubwa baada ya watu wengi kujihusisha zaidi na vita kuloko jambo lingine hivyo sekta ya michezo nayo iliadhirika kwa kiasi kikubwa.


Baada ya kuona hayo, kikosi cha Klabu ya Juventus kiliimarishwa na kuchukua wachezaji kadhaa mahiri ambao wengi walikuwa wakicheza katika kikosi cha kwanza cha timua ya Taifa ya Italia, ambapo baadhi yao alikuwa Giampiero Combi ambaye alikuwa ni mlinda mlango na aliyekuja kuwa shujaa kutokana na umahiri wake wa kumiliki mikiki mikiki ya safu ya usambualiaji ya timu pinzani, katika kipindi hicho timu hiyo ilikuwa chini ya Rais Corradino Corradini.

Kutokana na mafanikio ya hali ya juu ya Klabu ilianza kupata neema kutoka kwenye makampuni tofauti tofauti lakini kampuni ambayo ilikuwa ya kwanza ilikuwa ni Fiat inayojihusisha na mashuala utengenezaji wa magari ambayo ilikuwa inamilikiwa na Edoardo Agnelli kutoka katika familia ya Agnelli ambayo pamoja na mambo mengine lakini ilifanikiwa kuimiliki Juventus kibiashara kuloko kampuni nyingine yoyote na kipindi hicho ilikuwa ni mwaka 1923.

Moja ya mambo muhimu yaliyochangia familia hiyo kumiliki Juventus kwa kiasi kukibwa ni kuwa na uwezo wa kumiliki Uwanja katika eneo la Villar Perosa Kusini Magharibi mwa Turin, ambao ulikuwa na vitu vyote muhimu vilivyokuwa vinatakiwa kuwepo Uwanja wa Klabu kubwa kama Juve.

Kutokana na kuwa na jeuri ya fedha iliaendelea kufanya usajili wa nguvu ambaio ulisaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa kutwaa taji la ligi kuu nchini humo, tangu masimu wa mwaka 1925-26 kufuatia kuitandika timu ya Alba Roma katika fainali. Tangu mwaka 1930-31,1934-35 Juventus ilitwaa mataji muhimu matano na kuandika historia mpya katika Klabu hiyo kwa kufanya hivyo kwani ilikuwa haijatokea kwa miaka mingi, na wakati huo ikiwa na Kocha Carlo Carcano ambaye alikuwa lundo la wachezaji machachari Raimundo Orsi, Luigi Bertolini, Giovanni Ferrari na Luis Monti.

Mwaka 1933, Juventus ilirejea katika uwanja wake wa nyumbani wa maarufu kama Stadio Benito Mussolini, ambao ulijengwa mwaka 1933 ikiwa ni maalum kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia ya mwaka 1934 wenye uwezo wa kubebe mashabiki 65,000 wakiwa wamekaa kwenye viti. Jina la uwanja huu ilitokana na Benito Mussolini ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Italia ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo wa Taifa la Italia.

Baada ya vita ya pili ya Dunia jina la Uwanja wa Benito Mussolini lilibadilishwa na kuitwa Edoardo's son Gianni Agnelli ikiwa ni heshima ya Rais wa Klabu hiyo ambaye aliitumikia Juventus kwa mafanikio kubwa na hii ilitokana kifo cha Kiongozi huyu mnano Julai 14 mwaka 1935. Ikiwa chini ya Kocha Englishman Jesse Carver ilitwaa mataji mbali mbali muhimu katika miaka 1949-50 na 1951-52.
1957 Juventus iliwasainisha Welshman John Charles na Italo-Argentine Omar Sivori, kwa ajili ya kuichezea timu hiyo na moja ya watu wachezaji wanaokumbukwa kwa muda mrefu ni pamoja na Giampiero Boniperti ambaye aliitumikia Klabu hiyo tangu mwaka 1946.

Katika kipindi hicho mipango yao ilikuwa ya mafanuikio makubwa kwani ilishinda taji la ligi kuu nchini humo maarufu kama Serie A mwaka 1957-58 na 1959-60.
Kutokana na ushindi wa aina hiyo Juventus ilikuwa ni Klabu pekee nchini Italia ambayo ilifikia rekodi ya aina yake baada ya kutunukiwa tunzo maalum ya mafanikio kwa wanamichezo ambayo ilikuwa inatoilewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri pekee iitwayo (Stella d'Oro al Merito Sportivo) wakati ambapo mchezji Omar Sivori alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya.

Mwaka 1957 Juventus iliwasainisha Welshman John Charles na Italo-Argentine Omar Sivori, kwa ajili ya kuichezea timu hiyo na moja ya watu wachezaji wanaokumbukwa kwa muda mrefu ni pamoja na Giampiero Boniperti ambaye aliitumikia Klabu hiyo tangu mwaka 1946. Katika kipindi hicho mipango yao ilikuwa ya mafanikio makubwa kwani ilishinda taji la ligi kuu nchini humo 'Serie A' mwaka 1957-58 na 1959-60.

Kutokana na ushindi wa aina hiyo Juventus ilikuwa ni Klabu pekee nchini Italia ambayo ilifikia rekodi ya aina yake baada ya kutunukiwa tunzo maalum ya mafanikio kwa wanamichezo ambayo ilikuwa inatolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri pekee iitwayo (Stella d'Oro al Merito Sportivo) wakati ambapo mchezji Omar Sivori alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya.


Baada ya Boniperti alipostaafu mwaka 1961, alistaafu akiwa ni mfungaji bora wa katika Klabu hiyo kwani hadi anang'atuka alikuwa ameshafunga magoli 182 katika kichuano yote ambayo alicheza akiwa na Juventus ikiwa ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote ndani kwa kipindi cha miaka 45.


Kati ya mwaka 1966-67 Juventus ilishinda taji la mwisho ikiwa na Heriberto Herrera kama Kocha mkuu wa timu hiyo ilikiwa ni mafanikio ya mwisho huku akiwa anamtegemea zaidi mlinzi Sandro Salvadore.

Juventus iliendelea kuwa kinara wa soka na nuru ya soka la Italia tangu mwaka katika miaka ya 70 ambapo ilishinda mataji mbali mbali katika mwaka 1971-72, 1972-73, 1974-75 na 1976-77, wakati huo kikosi cha timu hiyo kilikuwa chini ya Kocha Cestmír Vycpálek, raia wa Czech aliyewahi kuichezea timu hiyo Juventus akiwa na wachezaji wengine mahiri katika wakati huo kama Gaetano Scirea, Roberto Bettega, Fabio Capello na Mbrazil José Altafini.

Lakini ukiachilia mbali suala hilo, pia Franco Causio alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa mahiri katika miaka ya 70.
Mwaka 1976- 1980, Juventus ilifanikiwa kutwaa majtaji muhimu ndani ya nje ya Italia likiwemo lile la Serie A, Klabi bingwa Ulaya, na UEFA lakini si hilo pekee lakini kubwa ni kuwepo kwa wachezaji waliotingisha medani ya soka katika wakati huo kama Marco Tardelli na Bettega.

Wakati huo Juventus ilikuwa chini ya Kocha Giovanni Trapattoni.
Katika kipindi cha miaka ya 1980 iliendelea kuwa tishio kwa kufanya kweli katika michuano mbali mbali ikiwemo ile ya Ligi kuu ya Italia yaani Serie A,ambapo ilishinda miaka ya 1980-81, 1981-82 na 1983-84. Klabu hiyuo iliendelea kuwa tishio katika michuano ya mbali mbali lakini michuano ambayo inakumbukwa hadi hivi leo ni ile ya fainali ya Kombe la Klabu bingwa barani Ulaya ambapo Juventus ilikutana uso kwa uso na Liverpool pambano lilochezwa katika Uwanja wa Heysel, huku Juve ikiibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0, lakini ikiwa ni fainali ya historia kwa kuwa ilisababisha vifo vya watu 39 na wengi wao wakiwa ni mashabiki wa Juventus Turin.

Katika kipindi cha miaka ya 90 Juventus kama ilivyo kwa Klabu yoyote ile imefanikiwa kusajili wachezaji mahiri wengi waliotamba wakiwa na Klabu hiyo kama vile Christian Vieri, Zinédine Zidane, Filippo Inzaghi na Edgar Davids. Waakati huo michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya ilipoanza ilishinda mataji ya ligi kuu nchini humo mara mbili, lakini pia ikiwa tishio kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya yaani mwaka 1997 na 1998 ikikumbana na timu za Borussia Dortmund ya Ujerumani, na Real Madrid ya Hispania.

Kufuatia kuwa nje ya Juventus kwa kipindi cha msimu mmoja Kocha Marcello Lippi alirejea ndani ya Turin lakini kurea kwake kulikuja sambamba na kuimarishwa kwa kikosi hicho kwa kuwanasa wachezaji kadhaa mahiri waliokuwa wanatamba kwenye ligi mbali mbali za Ulaya na kwingineko barani Ulaya, na kati ya wachezaji hao ni Gianluigi Buffon, David Trézéguet, Marcelo Salas, Pavel Nedved na Lilian Thuram.


Kutoakana kuwajaza wachezaji nyota duniani Juventus iliendelea kuwa juu katika soka la Italia kufuatia kutwaa taji la ligi kuu nchini humo maarufu kama Serie A katika msimu wa mwaka 2001-02 na 2002-03 ikiwa ni moja ya mafanikio ya kuwepo kwa nyota hao wa Dunia, lakini baadaye aliachana na klabu hiyo kisha kupewa mikoba ya timu ya Italia kwa ajili fainali za michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2006 iliyofanyika nchini Ujerumani.


Mwaka 2004, mchezaji wa zamani wa timu ya Juventus, Fabio Capello alichukua mikoba ya Lippe na kufanikiwa kutwaa mataji mengine mawili katika misimu miwili ya ligi ya Serie A. Lakini akiwa ni moja ya makocha wenye bahati mbaya katika maisha yake alikumba na mkasa wa maisha yake kisoka kwani May mwaka 2006, akiwa na Juventus alishudia timu yake ikishushwa daraja kutoka daraja la ligi kuu nchini humo Serie A hadi Serie B, lakini si hiyo pekee lakini kulikuwa na klabu nyingne kama AC Milan, Fiorentina, na Lazio ikiwa ni adhabu kutoka kwa chama cha soka nchini Italia kwa sababu ya tuhuma za upangaji wa matokeo katika ligi kuu.

Kutokana na tatizo hilo Kocha Capello, alirejea tena nchini Hipania katika klabu ya Real Madrid ikiwa ni hatua ya kukwepa fedheha kwa kufundisha timu iliyo daraja la pili kitu alichooinekana kutokipendelea kutokea maishani mwake. Licha ya kuondoka kwa Capello lakini Juventus ililazimika kukubali kuwaachia wachezaji kadhaa mahiri akiwepo aliyekuwa mlinzi wa kutumainiwa wa klabu hiyo anayechezea anache timu ya Taifa ya Italia, Fabio Cannavaro na kuelekea nchini Hispania kujiunga na timu ya Real Madrid.

Ikumbukwe kwamba Cannavaro ndiye mchezaji bora wa mwaka jana aliyechaguliwa na shiriksiho la soka duniani 'FIFA'.
Pia walikuwepo wachezaji kadhaa waliokuwa na uzalendo wa hali ya juu na klabu hiyo akiwemo Gianluigi Buffon, Nahodha Alessandro Del Piero, Pavel Nedved, Mauro Camoranesi na David Trézéguet. Kubakia kwa wachezaji hawa ndani ya Juve kuliongeza hamasa kwa wachezaji wachanga ambayo ndiyo ilikuwa chachu ya kurejea kwenye ligi kuu ya Serie A.

Dondoo nyingine muhimu kuhusiana na Juventus Turin, tangu kuanzishwa kwake. Huu ni mlolongo wa Marais waliowahi kuiongoza Klabu ya Juventus tangu kuanzishwa kwake.

Jina Mwaka
Eugenio Canfari 1897–1898
Enrico Canfari 1898–1901

Carlo Favale 1901–1902
G
iacomo Parvopassu 1903–1904

Alfredo Dick 1905–1906
Carlo Vittorio Varetti 1907–1910
Attilio Ubertalli 1911–1912

Giuseppe Hess 1913–1915
Fernando Nizza 1915–1918

Corrado Corradini 1919–1920

Gino Olivetti 1920–1923

Edoardo Agnelli 1923–1935

Giovanni Mazzonis 1935–1936

Emilio de Divonne 1936–1941

Pietro Dusio 1941–1947

Giovanni Agnelli 1947–1954

Marcello Giustiniani 1954–1955

Umberto Agnelli 1955–1962

Vittore Catella 1962–1971

Giampiero Boniperti 1971–1990

Vittorio Chiusano 1990–2003

Franzo Grande Stevens 2003–2006

Giovanni Cobolli Gigli 2006 aliyepo sasa

Makocha mbali mbali walioifundisha Juventus tangu mwaka 1923.

Jina Taifa Mwaka
Jeno Karolý Hungary 1923–1926

József Viola Hungary 1927–1929

George Aitken Scotland 1929–1930
Carlo Carcano Italia 1930–1935

Virginio Rosetta Italia 1935–1938

Umberto Caligaris Italia 1938–1940

Federico Munerati Italia 1940–1942

Felice Placido Borel Italia 1942–1946

Renato Cesarini Italia 1946–1947

William Chalmers Scotland 1948–1949

Jesse Carver England 1949–1951
Luigi Bertolini Italia 1951

György Sárosi Hungary 1951–1953
Aldo
Olivieri Italia 1953–1955

Sandro Puppo Italia 1955–1957

Ljubiša Brocic Serbia 1957–1959

Teobaldo Depetrini Italia 1959

Renato Cesarini Italia 1959–1961

Carlo Parola Italia 1961

Carlo Parola Italia 1961–1962

Paulo Lima Amaral Brazil 1962–1964

Eraldo Monzeglio Italia 1964

Heriberto Herrera Paraguay 1964–1969

Lùis Carniglia Argentina 1969–1970

Ercole Rabitti Italia 1970

Armando Picchi Italia 1970–1971

Cestmír Vycpálek Czech 1971–1974

Carlo Parola Italia 1974–1976

Giovanni Trapattoni Italia 1976–1986

Rino Marchesi Italia 1986–1988

Dino Zoff Italia 1988–1990

Luigi Maifredi Italia 1990–1991
Giovanni Trapattoni Italia 1991–1994

Marcello Lippi Italia 1994–1999
Carlo Ancelotti Italia 1999–2001

Marcello Lippi Italia 2001–2004

Fabio Capello Italia 2004–2006

Didier Deschamps Ufasansa 2006–2007

Giancarlo Corradini Italia 2007

Claudio Ranieri Italia 2007– Aliyepo sasa


Makampuni ya liyowahi kuidhamini Junventus tangu mwaka 1889.
Mwaka Mdhamini.

1981–1989 Ariston
1989–1992 Upim
1992–1995 Danone
1995–1998 Sony (Sony Minidisk)
1998–1999 D+Libertà digitale / Tele+
1999–2000 CanalSatellite / D+Libertà digitale / Sony
2000–2001 Sportal.com / Tele+
2001–2002 FASTWEB / Tu Mobile
2002–2004 FASTWEB / Tamoil
2004–2005 Sky Sports / Tamoil
2005–2007 Tamoil
2007–New Holland (Fiat) iliyopo sasa.

Orodha ya Kampuni mbali mbali ambazo zimetoa vifaa vya michezo kwa Juventus tangu mwaka 1979.

Mwaka Kampuni
1979–2000 Kappa
2000–2001 Ciao Web / Lotto
2001–2003 Lotto
2003– Nike iliyopo sasa.



Taifa N. anayocheza Jina la mchezaji

1 Italia Kipa Gianluigi Buffon
2 Italia Mlinzi Alessandro Birindelli (Makamu nahodha)
3 Italia Mlinzi Giorgio Chiellini
4 Argentina Mshambuliaji Sergio Bernardo Almirón
5 Ufaransa Mlinzi Jonathan Zebina
6 Italia Kiungo Cristiano Zanetti
7 Bosnia Kiungo Hasan Salihamidžic
8 Italia Kiungo Mauro Camoranesi
9 Italia Mshambuliaji Vincenzo Iaquinta
10 Italia Mshambuliaji Alessandro Del Piero (Nahodha)
11 Czech Rep. Mshambuliaji Pavel Nedved (Makamu nahodha)
12 Italia Kipa Emanuele Belardi
14 Uholanzi Mlinzi Jorge Andrade
17 Ufaransa Mshambuliaji David Trézéguet
18 Ufaransa Mlinzi Jean-Alain Boumsong
19 Italia Mshambuliaji Domenico Criscito
20 Italia Mshambuliaji Raffaele Palladino
21 Czech Rep. Mlinzi Zdenek Grygera
22 Australia Kipa Jess Vanstrattan ( amesajiliwa kwa mkopo kutoka Verona)
23 Italia Kiungo Antonio Nocerino
24 Uruguai Kiungo Ruben Olivera
28 Italia Mlinzi Cristian Molinaro
30 Uholanzi Kiungo Tiago
31 Italia Kipa Cristiano Novembre
32 Italia Kiungo Marco Marchionni
33 Italia Mlinzi Nicola Legrottaglie

Huu ndio undani wa klabu ya Juventus ya Jiji la Turin nchini Italia ikiwa ni klabu yenye historia yake iliyopitia kwenye mikimiki mingi yenye shida na raha yenye furaha na karaha.

Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wanaokipiga katika Klabu ya Juvenyus Turin, ya Italia.






















Nashukuru kwa kutembelea Blog hii, kazi njema lakini sisite kutoa maoni yako juu ya lolote kuhusiana na Blog hii.