Sunday, December 16, 2007

Unajua kilichotokea katika tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa gazeti la Championi mwaka 2008.

Mratibu wa shindano la mwanasoka bora wa mwaka wa gazeti la Championi 2007, Ahadi Kakore (katikati) akitangaza matokeo ya shindano hilo mbele ya waandishi wa habari hivi karibuni, kushoto ni Mhariri Isaac Kijoti na kushoto ni mhariri Denis Fusi.

Friday, November 16, 2007

Wachezaji England wamkaanga McClaren

Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Steve McClaren akisisitiza jambo kwa wachezaji. (Picha kwa hisani ya mtandao wa chama cha soka cha England FA.)

London, England

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya England wamemkaanga Kocha Mkuu wa timu hiyo, Steve McClaren baada ya kusema wazi kuwa hawawezi kupigana kwa ajili ya kutetea kibarua cha kocha wao.

Wachezaji hao wamesema kwamba licha ya umuhimu wa kufuzu mchezo ujao dhidi ya Crotia lakini hawatacheza kwa nje ya uwezo wao ili kulinda kibarua cha McClaren japo watajitahidi ili lengo la kulinda heshima ya nchi litimie.

Pia walisema kwamba hawatachukua jukumu la kuomba chama cha soka nchini humo (FA) ili McClaren aendelee kuinoa timu hiyo kwa sababu kile ambacho wapenda soka walihitaji hajakifanya.

Michael Owen alisema:Hatuwezi kubebena kiasi hiki lakini tunakachokifanya ni kulinda heshima ya nchi na si heshima ya mtu mmoja mmoja."

Naye Steven Gerrard alisema kwamba: Lakini jambo la msingi ni kulinda heshima ya Waingereza mbele ya mashabiki wa soka kote Ulimwenguni"

“Inajulikana wazi kuwa jukumu la timu kushinda halipo kwa wachezaji pekee, lakini kocha ana nafasi yake hivyo kama ameshindwa kutekeleza kile kinachotakiwa ni lazima awajibike kama ambavyo mtu mwingine anaweza kuwajibika akifanya isivyotarajiwa na wengi." alisema Peter Crouch.

England inakabiliwa na kibarua kigumu wakati itakapocheza na timu ya Taifa ya Crotia ikiwa ni moja ya mchezo wa kufuzu katika michuano ya Euro mwakani lakini ikiwa katika wakati mgumu wa kufuzu ikilinganishwa na timu nyingine kutoka katika kundi hilo ambazo ni Ujerumani, Israel, na Croatia.

Wigan yamlilia Bruce

London, England

Mwenyetiki wa klabu ya Wigan Athletic, Dave Whelan amesema kwamba anasubiri majibu kutoka kwa klabu ya Birmingham City kufuatia ombi la kumtaka Kocha Steve Bruce.

Whelan alisema kwamba Kocha huyo ameonesha mafanikio na watafanya kila liwezekalano ili Bruce anatua kwenye klabu hiyo.

“Tumeangalia kwa makini na tumegundua kwamba kuna uwezekano wa kufanya vizuri kama alivyofanya akiwa na Birmingham City hili ndilo linalotuumiza vichwa” Whelan aliliambia shirika la habari la Uingereza BBC.

Steve Bruce (46) anasakwa kwa udi na uvumba na tajiri wa Wigan Athletic raia wa Hong Kong, Carson Yeung ili kurejeshwa kuinoa Wigan Athletic.
.

Thursday, November 15, 2007

Eto’o awazia CAN 2008

Barcelona, Hipania

Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto’o anawazia michuano ijayo ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika nchini Ghana iwapo atakuwemo kwenye kikosi cha nchi hiyo au la.

Mshambualiaji huyo alisema kwamba japo hajui majaliwa yake katika michuano hiyo, lakini anawazia kulinda heshima ya Taifa lake katika michuano hiyo.

“Sijui lolote kama nitafanikiwa kucheza CAN ya nchini Ghana lakini mbivu na mbichi zitajulikana siku chache zijazo baada ya kurekebisha baadhi ya mambo yangu muhimu.

“Nitachokihitaji mimi ni kuona heshima ya nchi inaendelea kulindwa na kuwa juu kama miaka yote inavyokuwa kwa maana hili ndilo kila mtu analilia kufanyika katika taifa lake” Eto’o aliuambia mtandao wa Eurosport.

Mshambuliaji huyo amekuwa benchi kwa muda mrefu kwa sababu ya kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara jambo lilofanya viongozi wa juu wa Klabu ya Barcelona anayoichezea kusema wazi kwamba hawatamruhusu kucheza kwenye fainali zijazo za Ghana.

(Samuel Eto'o wa Cameron ambaye anawazia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2008 nchini Ghana.)

Euro 2008

Vigogogo roho juu

(Fabio Cannavaro wa Italia)
(Rood Van Nistelrooy wa Uholanzi)

London, England

Vigogo wa soka Barani Ulaya hivi sasa vipo roho juu juu, kufuatia hofu ya kufuzu michuano ya Ulaya mwakani ‘Euro 2008’ kutokana na upinzani ulipo.

Kesho katika viwanja mbali mbali barani humo kutakuwa na michezo kadhaa ya kuwania tiketi ya kucheza michuano hiyo ambapo baadhi ya timu kubwa za soka barani humo zitakuwa vitani kuwania pionti tatu muhimu.

Katika mechi za kundi B, Scotland itakuwa na kibarua kigumu ikiwa nyumbani dhidi ya Italia ambayo pia ina nafasi nzuri ya kusonga mbele kama itafanya vizuri kwenye mchezo huo.

Nayo Israel ikiwa katika kundi E, itakuwa na kazi ya ziada kutetea ushindi wake wa nyumbani pale itakaposhuka dimbani ikipepetana na Urusi ambao wanaonekana kuwa na kikosi imara ambacho ni tishio katika kundi hilo.

Ujerumani ikiwa nyumbani itatakiwa kulinda heshima ya uwanja wa nyumbani kwani itahitaji ushindi wowote mbele ya Cyprus katika mchezo wa kundi D.

Vigogo wengine barani humo, Uholanzi nayo itataka kuonesha umwamba wake mbele ya washabiki wao watakapowakaribisha Luxembourg mchezo ambao unatabiriwa kuwa mgumu hivyo Wadachi hao hawatategemea mteremko katika mchezo huo, huku Slovakia watakuwa wageni wa ndugu zao wa Jamhuri ya watu wa Czech.

Katika michuano hiyo pia kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka katika kundi A, pale Poland itakapoikaribisha Ubelgiji wakati mchezo mwingine wa kundi hilo utakuwa kati ya Kazakhstan wataokuwa wageni wa Serbia.

Mchezo wa kundi A ambao unatazamiwa kuwa mgumu zaidi ni pale Ureno itakaposhuka katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Armenia, wakati katika kundi F, shughuli itakuwa pevu pale Sweden watakapokaribishwa nyumbani kwa Hispania mchezo unaotarajiwa kuwa wa nguvu, hiyo ndiyo hali ilivyo katika michezo ya kufuzu Euro 2008.

Friday, November 9, 2007

Kombe la Dunia 2014 litafunika-Pele

Huyu ndiye yule mfalme wa soka Duani, Edson Arentes do Nascimento 'Pele'

Brasilia, Brazil

Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Brazil, Edson Arentes do Nascimento maarufu kama Pele, amesema kwamba michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2014, 'itafunika' itavunja rekodi ya michuano mingine iliyopita.

Pele amesema kwamba atatumia uwezo wake wote kuhakikisha kwamba anaitangaza Brazil katika kipindi chote cha maandalizi ya michuano hiyo ambayo mwaka 2014 itafanyika nchini Brazil.

"Michuano ya 2014 itavunja rekodi, kwani haijawahi kutokea kamwe, mimi kama balozi, nitaitangaza nchi yangu kwa nguvu zote na kushirikiana bega kwa benga na serikali, shirikisho la soka la Brazil 'CBF' pamoja na wadau wengine humihu ili kuweka mambo sawa kabla ya kuanza kwa michuano." Alisema Pele.

Brazil hivi karibuni ilisema kwamba, itawatumia wanasoka wake wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya pamoja na wale waliostaafu siku nyingi akiwemo Pele, ili kuitangaza nchi hiyo kimataifa zaidi.

Mshike mshike Klabu bingwa barani Ulaya 2007

Man United, Barca zaua,
Arsenal yapaa Ronaldo,
Rooney, Tevez wameremeta

London England

Kivumbi cha Ligi ya mabingwa barani Ulaya kiliendelea tena, usiku wa kuamkia jana katika viwanja mbalimbali ambapo timu ya Manchester United, ikiwa nyumbani ilipata ushindi mnono baada ya kuitandika Dynamo Kiev bao 4-0.

Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Old Trafford, ambapo makosa yaliyofanywa na walinzi wa Dynamo yalisababisha kuleta zahama kwa timu hiyo, baada ya mchezaji wa Manchester United, Pique kuandika bao la kwanza katika dakika ya 31 ya mchezo.

Bao hilo liliongeza hamasa ya mashambulizi kwa Manchester United, jambo lililofanya washambuliaji wake kama Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney, kutumia makosa madogomadogo hivyo kuongeza bao la pili lililofungwa na Carlos Tevez katika dakika ya 37. Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Manchester United ilikuwa mbele kwa bao 2-0.

Katika kuonesha kwamba mwaka huu Mashetani Wekundu hao, walikuwa na uchu wa kufika mbali, Wayne Rooney aliwanyanyua tena mashabiki wake kwenye viti, baada ya kuandika bao la tatu katika dakika ya 76.

Pamoja na ushindi huo mnono lakini haikutosha kwani Mreno Cristiano Ronaldo, alihitimisha karamu ya mabao kwa Machester United, baada ya kufunga bao la nne katika dakika ya 88. Hivyo hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Manchester United bao 4 na Dynamo Kiev 0.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, timu ya Barcelona ya Hispania ilitoka na ushindi mnono wa bao 2-0 dhidi ya Rangers, mchezo ambao Barca ndio walikuwa wenyeji.

Bao la kwanza kwa upande wa Barcelona lilipatikana katika dakika ya saba ya mchezo, kupitia kwa mshambuliaji mwenye kasi, Thierry Henry.

Mchezo huo uliendelea huku Barca wakiwa wapo juu, kuliko wageni wao jambo lilifanya mchezo kuelemea upande mmoja, licha ya kwamba kulikuwa na mashambulizi ya kustukiza langoni kwa Barcelona.

Hali hiyo ilimlazimisha Kocha wa timu hiyo, Frank Rijkaard kusimama na kuhamasisha vijana wake na kusababisha kupatikana bao la pili, kupitia kwa Lionel Messi aliyefunga katika dakika ya 43 ya mchezo akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mbrazil Ronaldinho Gaucho.

Pamoja na matokeo hayo lakini kulikuwa na mchezo mwingine, ambapo timu ya Lyon ikiwa nyumbani ilitoka na ushindi mnono wa bao 4-2 dhidi ya timu ya Stuttgart.

Mabao ya Lyon yalifungwa na Ben Arfa katika dakika ya sita na 37, hivyo kuonekana kwamba kulikuwa na matumaini mapya ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Naye mchezaji Källström aliifungia Lyon bao la pili katika dakika ya 15 ya mchezo, wakati dakika ya 90 ya mchezo Juninho alifunga mlango wa mabao kwa timu yake baada ya kuandika bao la nne.

Licha ya Lyon kupata mabao hayo lakini Stuttgart Gomez ilijitutumua na kuandika mabao mawili ya kufutia machozi yaliyoandikwa na Gomez katika dakika ya 16 na 56.

Wakati huo huo Slavia Praha ilishindwa kutamba nyumbani na kuruhusu kugawana pointi na Arsenal, hivyo matokeo ambayo yaliwezesha watoto Mfaransa Arsene Wenga kupata kupita na kutua hadi kwenye hatua ya mtoano.

Wakati hayo yakiendelea lakini kwa upande wa Kocha wa Liverpool, Rafael Benitez amesema kwamba, baada ya kutoa kipigo cha Mbwa mwizi kwa baada ya kuichapa Besiktas ya Uturuki kwa bao 8-0, anaangalia ni vipi ataweza kuifunga Futebol Clube do Porto, maarufu kama FC Porto ya Ureno wakati, huku vijongoo hao wa Anfield watakapokuwa ugenini katika Uwanja wa Estádio do Dragão jijini Lisbon Ureno. Mchezo huo baina ya FC Porto na Liverpool utashudiwa na mashabiki wapatao 50,476.

Marta Vieira da Silva

Nguli anayewazimia Gaucho,

Rivaldo
LA Galaxy wamtangazia vita

Karibu mpenzi msomaji wa safu hii ya wanamichezo bora na maarufu duniani, ambapo kama ilivyo ada ya gazeti la Championi hukuletea taarifa za wanamichezo wanaovuma kwa sasa ikiwemo wa mchezo wa soka.

Leo katika safu hii kuna zawadi ya Krismasi na Mwaka mpya kwani tunaye mwanasoka wa kike kutoka nchini Brazil, Marta Vieira da Silva. Marta alizaliwa tarehe 19, Februari mwaka 1986 katika eneo la Dois Riachos, jimbo la Alagoas, Brazil.

Baba mzazi wa Marta ni Aldário Vieira da Silva na Mama yake anaitwa Tereza.Familia hiyo imejaliwa kuwa na watoto wanne ambao ni Martha mwenyewe na ndugu wengine watatu ambao ni José, Valdir na Angela.

Tangu akiwa mtoto kipaji chake cha kusukuma kandanda kilianza kuonekana na kuwa juu wakati wa mashindano mbali mbali ya soka kwa shule za msingi, ambayo yalishirikisha Wasichana wenye umri mdogo.

Katika heka heka hizo za kutafuta timu za vijana makocha waliweza kuvutiwa vilivyo na kiwango cha mchezaji huyu, hivyo kuanza vita ya kumgombea ili kuzichezea klabu zao.

Mafanikio ya Marta katika ulimwengu wa soka la Kimataifa uliianza kuonekana tangu mwaka 2004 wakati wa michuano ya Olympic ambayo iliwashirikisha wachezaji mbali mbali wa kike duania ambapo yeye alikuwa na umri wa miaka 19.

Mafanikio machache ambayo yanaelezwa ilikuwa ni kutwaa medali ya fedha 'silver' katika michuano ya Olympic ya mwaka 2004, huku akifumania nyavu mara sita. Mwaka 2006 Martha alishinda yuzo ya wanasoka bora wa kike wa shirikisho la soka duniani iitwayo 'FIFA Women's World Player of the Year'.

Mwaka uliofuata yaani 2007 katika fainali ya michuanoa ya Kombe la dunia, mwanadada huyu alishinda tuzo mbili muhimu amabazo ni mpira wa dhahabu 'Golden Ball award' akiwa ni mchezaji bora wa mashindano lakini pia alitunukiwa kiatu cha dhahabu 'Golden Boot award' baada ya kuwa mfungaji bora wa mwaka wa Kombe la Duniani la Wanawake.

Pamoja na hayo lakini alitwaa kiatu cha dhahabu ikiwa ni mchango wake katika timu ya Taifa kwenye michianio hiyo ambapo aliotwa zawadi hiyo kama mchezaji bora wa kike wa shirikisho la soka duniani FIFA.

Kwa upande wa ngazi ya klabu, Marta alijiunga na klabu mbali mbali akianzia nchini kwao katika ya Vasco da Gama mwaka 2000-2002 akicheza kwenye kikosi cha timu ya Vijana ya klabu hiyo.

Baada ya kupata mafanikio kwenye klabu hiyo wamiliki wa klabu ya Santa Cruz ya nchini Brazil iliona kipaji chake na kuanza kufanya mikakati ya kumtwaa na hapo alijiunga moja kwa moja kwenye kikosi cha wakubwa baada ya kusota kwenye timu ya Vijana, hapo ilikuwa ni mwaka 2002.

Mwaka 2004 Martha alipata ofa nyingine iliyokuwa ya maana kubwa kwake ambapo alijiunga kwenye kikosi cha timu ya Umeå IK, timu ambayo anaendelea kuitumikia hadi muda huu.

Oktoba mosi mwaka huu baadhi ya klabu kubwa duniani zimeanza hekaheka za kumtwaa Martha ambapo bado mipango inaendelea kwa kasi, huku baadhi yake zikidai kwamba zipo tayari kumng'oa mchezaji huyo kwa gharama yoyote ile.

Moja wapo ya klabu ambazo zimeonesha nia ya kutaka kumtwaa Martha ni pamoja na Los Angeles Galaxy ya marekani, ambayo imeahidi kufanya kila liwezekanano kuhakikisha kwamba uhamisho wa nguli huyo unafanyika muda mfupi kuanzia sasa.

Hivi karibuni Martha alifanya mahojiano na Jarida la Four Four Two na nchini Uingereza ambapo katika mahojiano hayo alifanikiwa kueleza masuala mbali mbali ya maisha yake lakini kuwa alillolieliza ni kwamba katika wanasoka wa Brazil wapo wawili ambao wanamvutia kwa kiwango kikubwa.

Aliwataja walikuwa wanamvutia na kufurahishwa na usakataji kandanda kuwa ni pamoja na Ronaldinho Gaucho anayekipiga katika klabu ya Barcelona ya Hispania pamoja na mchezaji wa zamani wa Brazil na Rivaldo.

Licha ya ukweli kwamba Martha ni mchezaji mzuri na anayeelewa vilivyo suala zima la soka, lakini kwa upande wa michezo mongine anapendelea zaidi mchezo wa tenesi na hutumia muda mwingi kuangalia michuano mbali mbali ya mchezo huo, ikiwemo kwenda kwenye vieanja au anapokosa nafasi basi hufuatilia kwenye Luninga.

Monday, November 5, 2007

Mjue Marta Vieira da Silva wa Brazil

Jina Kamili: Marta Vieira da Silva
Tarehe ya Kuzaliwa: 19 Februari 1986
Miaka: 21
Mahali pa kuzaliwa: Dois Riachos, Alagoas, Brazil
Urefu: 1.62 m
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji
Klabu anayocheza:Umeå IK, sweden
Namba ya jeszi:60
Klabu ya Vijana: Vasco da Gama(2000-2002)
Klabu ya wakubwa: Santa Cruz (2002-2004)
Umeå IK:2004

Saturday, October 20, 2007

Picha zote kwa hisani ya mtandao wa Lucky Dube

Lucky Philip Dube

Mtetezi wa wanyone aliyezimika kama mshumaa

MWANAMUZI Lucky Philip Dube alizaliwa, Agosti 3, 1964 nchini Afrika Kusini katika eneo la Ermelo, mashariki mwa Eastern Transvaal kwa sasa eneo hilo linaitwa Mpumalanga.

Wakati mama yake akiwa na ujauzito wake, wazazi wake walitengana, baada ya kuzaliwa alionekana kwamba hatoweza kuishi muda mrefu kwa sababu alikuwa na matatizo ya kiafya, hivyo kutokana na tatizo hilo mama yake alimpa jina la Lucky, likimaanisha Bahati.

Lucky Dube alikulia mikononi mwa mama yake mzazi aitwaye Sarah, lakini Bibi yake mzaa mama ndiye aliyekuwa na jukumu la kumlea kwani mama yake alikuwa akitumia muda mwingi kwenda kutafuta riziki ili aweze kulea familia yake ambayo ilikuwa na watoto watatu kwa wakati huo ambao ni Thandi, Patrick na Dube.

Kutokana na ugumu wa maisha ulioikumba familia yao, Lucky Dube hakufanikiwa kupata elimu kwa wakati unaotakiwa, hivyo alilazimika kuhama kutoka eneo alikozaliwa na kwenda kuishi katika jiji la Durban ili kutafuta maisha.

Chanzo cha yeye kushindwa kupata elimu kwa wakati kulitokana na siasa za ubaguzi wa rangi zilizowagawa watu katika makundi ambayo ni Wazungu, Waarabu na Wahindi kisha Weusi, hivyo hata huduma muhimu kama elimu na matibabu kwa Waafrika ilikuwa sio lazima.

Akiwa Durban, Dube alifanya kazi za utunzaji wa bustani za wazungu jambo lililosaidia kupata kipato kidogo ambacho alikigawa kwa familia yake, kiasi kingine kikibakia kwenye mikono yake kwa ajili ya kulipia ada ya shule na kumsaidia kwenye masuala ya maisha.

Huko alikwenda shule na kukutana na baadhi ya watu ambao walikuwa na vipaji vya muziki na kuunda urafiki kisha walijiunga na kuanzisha kwaya ambayo iliweza kutunga wimbo wa shule waliouita 'The Skyway Band'.

Wakiwa shuleni vugu vugu la kupigania uhuru lilipanda ambapo waliazisha kundi lililojukana kama 'Rastafari movement' ambapo lilipata umaarufu na kukubalika kwa kuwa kulikuwa na nyimbo kadhaa ambazo zilikuwa za kuwatetea watu wanyonge na waliokuwa wanakandamizwa na serikali ya kibaguzi wakati huo.

Alipofikisha umri wa miaka 18, Lucky Dube alijiunga na bendi iliyokuwa inajukana kama The Love Brothers ambayo ilifanya kazi kubwa kuwaelimisha watu weusi juu ya masuala mbalimbali ikitumia mtindo wa Kabila Kizulu ikiitwa Mbaqanga, bendi ambayo ilikuwa chini ya kampuni ya Tear Records.

Baada ya kutoa Albamu ya tano na kundi hilo mwanamuziki huyo alijikita kwenye muziki wa Reggae ambao kipindi hicho ulianza kuwa na soko kubwa nchini humo baada ya kugundulika kwamba ndiyo ambao ulikuwa na ujumbe mzito uliofika upesi kwa jamii husika huku akimuangalia zaidi Marehemu Peter Tosh wa Jamaica ambaye alikuwa aking'ara kwa miondoko hiyo.

Mwaka 1984, Lucky Dube alitoa albamu yake ya kwanza iliyokuwa inajukana kama 'Rastas Never Die'. Licha ya kufanikiwa kuingiza sokoni, haikufanya vizuri kama ambavyo alitarajia.

Mwaka 1985, mwanamuziki huyo alingia studio na kutoka na kitu kipya kilichokuwa kinajukana kama 'Think About The Children'. Kutokana na ujumbe uliokuwemo kwenye albamu hiyo, iliweza kumtangaza vema kwenye ulimwengu wa muziki kwani alianza kuvuma nje na ndani ya Afrika Kusini.

Alikaa miaka kadhaa bila kutoa albamu hadi mwaka 1989 ambapo alishinda tuzo tofauti ikiwemo ile ya kituo cha Runinga, iitwayo 'OKTV Awards', hivyo kufanya baadhi ya makampuni makubwa ya kurekodi kuanza kumnyemelea, Mwaka 1995 Kampuni ya Motown ikafanikiwa kumpata nyota huyo.

Mwaka 1996 aliweza kutoa albamu ya mjumuisho ambayo ilifanya vizuri na kunyanyuka zaidi ya alivyokuwa anategemea hivyo kuendelea kuwa juu katika muziki huo wa Raggae Duniani kwani alitunukiwa tuzo mbalimbali kubwa kama ile ya "International Artist Of The Year" iliyotolewa na Ghana Music Awards (Ghana).

Mwanamuziki huyo licha ya kujikita katika muziki aliendelea na masomo ambapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal na kufanikiwa kupata shahada ya kwanza katika sayansi (BSC), kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha Wits na kupata shahada ya pili. (Masters).

Lucky Dube aliwahi kukumbwa na tuhuma za kuhusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa wapiga 'dram' wake aitwaye Senzo ambaye alikuwa msanii kinda katika muziki wa Reggae nchini humo ilidaiwa kwamba alituma watu ili kumua kijana huyo kwani alikuwa ameanza kuja juu katika muziki huo na kumpora mashabiki.

Kutokana na tuhuma hizo heshima ya mkongwe huyo wa Raggae iliporomoka ndani ya jamii ya Waafrika Kusini hasa wale waliokuwa wanapigania uhuru na haki nchini humo, kwani msanii huyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliochangia kupatikana mafanikio makubwa ya ushindi dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Lakini mwanamuziki huyo alijibu kwa kusema "Mimi ni mtu safi, damu ya Senzo haipo mikononi mwangu naamini ukweli utajulikana, kama siyo leo basi itakuwa kesho na hata kama sitokuwepo basi watakaokuwepo watajua ukweli huo".

Lakini Oktoba 18, 2007, ndiyo siku ambayo wengi wa mashabiki wa muziki wa Raggae hawawezi kusahau kamwe kwani Dube aliuawa katika shambulio la Risasi lililofanywa na majambazi watatu katika eneo la Rosettenville nje kidogo ya jiji la Johannesburg.

Baada ya kifo cha Dube nchi mbalimbali hasa za Afrika zilipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa, huku baadhi ya mashabiki wakisema kwamba nuru ya muziki wa Reggae duniani imetoweka.

Nchi kama Ghana, Nigeria, Ghana Tanzania na Afrika Kusini kwenyewe baadhi ya vituo vya redio na Runinga vilisikika vikiendesha vipindi maalum ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kifo cha staa huyo.

Baada ya kifo hicho Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, alitoa kauli nzito na kuagiza vyombo vya dola kuwatafuta walihusika kwa udi na uvumba hadi wapatikane ili sheria ichukue mkondo wake. Taarifa hiyo iliambatana na rambirambi kwa familia ya Dube.

Baadhi ya nyimbo zake zilizotia fora na mwaka wa kutunga katika mabano ni
Rastas Never Die (1984)
Think About The Children (1985)
Slave (1987)
Together As One (1988)
Prisoner (1989)
Captured Live (1990)
House of Exile (1991)
Victims (1993)
Respect (2006).

=====================

=====================

Saturday, October 13, 2007

Aliyemsafi Yanga awe wa kwanza kurusha jiwe

Na Ahadi Kakore

KWANZA napenda nimshukuru Mungu muweza wa yote kwa wema na fadhila zake kwangu, hasa kwa kuniwezesha kufika wakati huu, nawajibika kusema hayo kwa sababu wapo wengi tuliokuwa nao siku, saa na dakika chache zilizopita lakini leo hii hawapo nasi tena.

Vile vile naomuomba Mwenyezi Mungu anijalie hekima ya kutosha na kuniwezesha kuandika yanayostahili katika uchambuzi huu ili ujumbe ufike kama nilivyokusudia, naamini sala yangu imesikika.

Baada ya kusema hayo, nirejee kwenye kiini cha mjadala, ambapo siku ya Jumatano wiki iliyopita Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega akiwa sambamba na Mhazini wao, Abeid Mohamed Abeid 'Falcon' pamoja na Katibu Mwenezi, Francis Lucas walilazimika kuitisha mkutano na wahariri wa vyombo vya habari za michezo nchini.

Mkutano huo uliitishwa na viongozi hao baada ya aliyekuwa mfadhili wa Yanga, Yusuf Manji kutangaza kujitoa kwenye ufadhili wake ndani ya klabu hiyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Manji alieleza kuwa sababu za kujitoa ni kutokana na viongozi wa Yanga kushindwa kutekeleza rasimu ya katiba kama walivyokubaliana awali.

Lakini baada ya kutangaza kujiondoa ndani ya Yanga, siku iliyofuata alirejea Jangwani akiwa ameambatana na kundi la wazee na baadhi ya wanachama. Hatua hiyo ilikuja baada wazee kumuangukia.

Katika mkutano huo na wahariri, Madega alifafanua kuwa mbegu ya kutoelewana na Manji ilianza kumea wiki moja baada ya kuchaguliwa kwao, baada ya mfadhili huyo kukutana na viongozi na kuwaeleza hatua ya kusaini mkataba ambao ungeifanya timu iwe chini ya Kampuni badala ya klabu.

Mageda alisema yeye hakukubaliana na hatua hiyo, tofauti na viongozi wengine "Binafsi nilihamaki sana kwa kuwa ninaamini mimi ni mtu mzima mwenye akili timamu, msomi na nina uwezo wa kawaida wa kuchanganua mambo na zaidi kitaalam mimi ni mwanasheria.

"Nalinda heshima yangu zaidi kuliko maslahi, hivyo kwa uwazi kabisa sikukubali kufanya vile, kama kiongozi mkuu hadi hapo katiba ya Yanga pamoja na muafaka wenyewe nitakapoupitia kikamilifu," ilisema taarifa ya Madega aliyoitoa.

Kadhalika taarifa hiyo ilisema kwamba katika katiba kuna upungufu kadhaa ambao ni muhimu kufanyiwa marekebisho kabla ya kuanza kwa mchakato wa kampuni.

Alifafanua baadhi ya vifungu vya katiba, kiwemo cha 39 (2) (d) kuwa kinauagiza mkutano mkuu wa uchaguzi, kuchagua wanachama wawili ambao si miongoni mwa viongozi wa klabu kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni kwa ajili ya kuwakilisha maslahi ya klabu katika kampuni.

Hivyo akasema kifungu hicho na vingine havina budi kufanyiwa marekebisho makubwa kabla ya kukubali kujitumbukiza katika kampuni.

Hayo yaliyosemwa na Mageda yawezekana yakawa na ukweli lakini naamini haikuwa kauli ya kukurupuka kwa sababu anaelewa madhara ya kufanya mambo kwa kukurupuka akiwa kama kiongozi mkubwa.

Kwa upande wa pili wa shilingi, tumeshuhudia Manji akijitoa huku akisisitiza kwamba hali ya mambo ilivyo hivi sasa ndani ya Yanga ndiyo yaliyosababisha kujiondoa kwake lakini akisisitiza kwamba rasimu ya katiba imekuwa haifuatwi.

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kuondokewa na mfadhili, kwani mwaka 1994, ilikimbiwa na wafadhili watano akiwemo Marehemu, Abbas Gulamali, wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa George Mpondela 'Castro'.

Ikumbukwe kwamba wakati Manji anaingia ndani ya Yanga kulikuwa na mgogoro mkubwa ambao watu mbali mbali walishindwa kuuzima. Mgogoro huo ulidumu kwa muda wa zaidi ya miaka mitano na kusababisha maendeleo ya klabu hiyo kuwa duni licha ya kwamba iliwahi kuibuka ubingwa ndani ya kipindi hicho.

Ni ukweli usiofichika kwamba pamoja na mataji yaliyopatikana katika wakati huo lakini mgawanyiko uliokuwepo uliigawa Yanga katika makundi matatu ambayo ni Asili, Academia na Kampuni.

Kutua kwa Manji mitaa ya Twiga na Jangwani kulisababisha mgawanyiko uliokuwepo kumalizika na kupatikana Yanga moja imara, sambamba na hilo kulifanyika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo mwezi Mei mwaka huu na kuwaweka madarakani viongozi waliopo hivi sasa.

Hali hiyo inanifanya kufunua Biblia Takatifu na kukutana na ujumbe kutoka katika kitabu cha Zaburi 125:4 ambao unasema "Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, nao walio wanyofu wa moyo".

Kwa upande wa Quruan Tukufu inasema "Innal hilah maswabirina' ikiwa na maana ya 'Hakika wenye kusubiri wapo pamoja na Mwenyezi Mungu'.

Kwa maana hiyo hoja zilizotolewa na pande zote mbili zinafaa kuchujwa na kutazamwa kwa macho mawili ili kumuondoa Bundi mbaya anayeweza kuifikisha klabu pabaya.

Nimeamua kutumia vifungu kutoka katika vitabu hivi kwa sababu binafsi naamini moja ya kitabu hicho lakini pia wengine wanaamini vitabu hivi katika maisha yao ya kila siku.

Hatukuzoea kuona wachezaji wa Yanga wakijihusisha na mgogoro ndani ya klabu, lakini kwa kipindi hiki tumeshuhudia yanatokea jambo ambalo ni hatari, kwani awali timu ikiwa ndani ya migogoro ilikuwa inatwaa vikombe kwa sababu wachezaji walikuwa wakijiepusha nayo.

Wito wangu kwa Wanayanga wote ni nawaomba wote wanaohusika na sakatala hili kuweka tofauti zao chini na kuangalia mbele kwa manufaa ya Yanga.

=========================================================
Vimbwanga vya mastaa

Rais asiyecheka Duniani

Pung Yang, Korea Kaskazini

Rais wa Jamhuri ya watu wa Korea Kaskazini, Kim Jong-il anasemekana kuwa ndiye kiongozi asiyependa kucheka ikilinganishwa na viongozi wengine duniani.

Kwa mujibu wa jarida moja la nchini humo,Kim Jong-il akiwa amefurahishwa na jambo huishia kutikisa kichwa au kunyanyua mikono na kuwapungia wananchi wake.

Imefahamika kwamba Kiongozi huyo anayefuata mlengo wa Kimonisti, amekuwa na tabia hiyo kwa muda mrefu jambo linalowafanya watu wengi ambao si raia wa nchi hiyo kushindwa kutambua wakati gani huwa na furaha.

Wachunguzi wa mambo wanadai kwamba watu wengi waishio nchini humo wameshindwa kufanikiwa kuyaona 'meno' ya kiongizi wao japo hata kwa bahati mbaya, jambo linalowafanya watu wengi kumwogopa.

Viongozi wa kijeshi nchi humo ndio waliobahatika kumwona Kim Jong-il akicheka kwa mara ya mwisho wakati alipotembelea kituo kimoja cha kijeshi nchini humo kushuhudia majaribio ya makombora ya masafa marefu jambo ambalo lililaaniwa Marekani.

=========================================================

Mapenzi yamchanganya Michel Jackson

Califonia, Marekani

Mwanamuziki wa miondoko ya Pop duniani, Michael Jackson, ameweka wazi kwamba mapenzi aliyopata kutoka kwa mfanyakazi wake wa ndani 'yaya' yalimdatisha.

Jackson alisema kwamba mwanadada Rose, alikuwa anampa mapenzi moto moto ambayo yalimchanganya kiasi kwamba alianza kufikiria namna ya kufunga naye ndoa.

"Ukweli Rose alinidatisha sana na penzi lake hilo halina ubishi, kiasi cha kufikia hatua ya kutaka kufunga naye ndoa wakati fulani japo haikufanikiwa, huo ndio ukweli wa uhisiano wangu na Rose" alisema Jackson.

Siku za nyuma iliwahi kuripotiwa kwamba, Jackson alikuwa akiwekwa kinyumba na mfanyakazi wake wa ndani, jambo alilolikanusha vikali na kuwakasirisha majirani zake waliokuwa wakidai Jackson alikuwa akiukataa ukweli.

=========================================================

J.Lo afuata nyayo za Madona

Alabama, Marekani

Mwanamuziki nyota wa R&B nchini Marekani Jenifer Lopez, amesema kwamba kama yupo mbioni kufuata nyayo za mwanamuziki mwenzake, Lady Madona.

Akizungumza katika kituo kimoja cha Luninga katika jimbo la Alabama nchini Marekani, Lopez 'J.Lo' alisema kwamba Madona ndiye mwanamuziki ambaye anamvutia kutokana na mtindo wa maisha yake wa kulea watoto wenye matatizo.

"Hata mimi nikifanikiwa kuweka mambo yangu sawa nitafanya kama alivyofanya Madona, wakati huu najipanga kwa ajili ya kuchukua watoto wawili ili niishi nao kama watoto wangu hili linawezekana" alisema J.Lo.

Madona alimchukua David Banda wa nchini Malawi kwa ajili ya kumlea kama mwanaye, lakini bado haijafahamika J.Lo atawachukua watoto kutoka sehemu gani duniani.

=========================================================

Rihanna; nasakwa usiku na mchana

London, Uingereza

Mwanamuziki Rihana wa Marekani aliyejipatia umaarufu katika miondoko ya R&B amesema kwamba anasakwa na wanaume wakware usiku na mchana ili kufanya nao ngono.

Msanii huyo alisema hayo wakati alipoulizwa na gazeti la The Sun la nchini Uingereza, ni kitu gani kinachomsumbua katika maisha yake ya ustaa.

"Maisha ya Ustaa ni tabu tupu hakuna asiyefahamu haya, mambo yanayonisumbua ni wanaume wanaonitafuta ili kufanya nao ngono" alisema Rihana.

Msanii huyo aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine lakini maisha ya aina hiyo ni magumu kwani anafuatiliwa sana, vikiwemo vyombo vya habari ambavyo kila siku vinataka kujua undani wa maisha yake.

Msanii huyo aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine lakini maisha ya aina hiyo ni magumu kwani anafuatiliwa sana, vikiwemo vyombo vya habari ambavyo kila siku vinataka kujua undani wa maisha yake. maisha yake.

mapenzi yamchanganya gaucho

Amini usiamini mchambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na Barcelona Ronaldinho Gaucho inasemekana kwamba bifu lilipo hivi sasa ni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti wa Kocha wake Frank Rijkaard.

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mwanasoka huyo zilisema kwamba uhusiano uhianza mapema mwaka jana kiasi cha kufanya kupunguza ari ya kufanya mazoezi.

Kutokana na hali hiyo baadahi ya watu walianza kumchunguza nguli huyo ambaye ndiye anayeongoza kwa kulipwa kitita kikubwa cha fedha kuliko mchezaji yeyote duniani, ambapo ilibainika kwamba biti wa Rijkaard mwenye miaka 20 ndiye chanzo cha mambo yote.

Hata hivyo baada ya kuibuka kwa taarifa hizo Rijkaard hakukubaliana na taarifa hiyo hivyo kujikuta akiingia kwenye bifu zito na nguli huyo kiasi cha kufanya kushindwa hata kusalimiana wakati mwingine.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Kocha huyo kusema wazi kuwa hatokubali mtu amharibie mwanae hivi hivi na atasimama kidete kutetea haki yake.

Duh! inakuwaje tuendelee kuwa soka ili kujua nini kitakachoendelea juu ya bifu hilo linalonekana kitingisha dunia kwa sasa.

Huyu ndiye Ronaldinho Gaucho a.k.a kidume cha mbegu kilichofanya uharibifu wa hali ya juu katika nyumba ya Rijkaard.

Huyu ndiye Baba wa binti anaitwa Frank Rijkaard.

---------------------------------------------------------------------------------------------

Saturday, October 6, 2007

Umeipata hii ya waamuzi wa bongo?

Waamuzi safi lakini hawa mh!

Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Simba Hassan Dalalali, alisema wazi kwamba kuna baadhi ya waamuzi wanaochezesha Ligi kuu Tanzania Bara, wamekuwa ni kikwazo kwa timu kadhaa kushindwa kufurukuta wanapokuwa kwenye viwanja vya Ugenini.

Inawezekana kauli ya Dalalali ikawa inaukweli fulani au ikawa haina ukweli wowote, lakini inalazimu kusema hayo kwa kuwa kuna baadhi ya viwanja huwa vinakuwa ni mwiba mchungu kwa timu ngeni.

Wote tunakumbuka Uwanja wa Ilulu ulioko mkoani Lindi ambao Timu ya Kariakoo ya mkoani humo ilikuwa ikiutumia kama uwanja wake wa Nyumbani.

Kumbu kumbu zinaonesha kwamba kati ya timu 10 zilizocheza katika uwanja huo ni timu tatu tu ambazo ziliweza kushinda ikimaanisha kwamba kati ya asilia 100 ya michezo yote iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ilulu ni asilimia 30 tu ambayo Kariakoo iliweza kufungwa.

Pia asilimia tano ndiyo pekee ambayo ilikuwa ni michezo ya sare huku asilimia iliyobakia ilikuwa Kariakoo ilishinda. Ushindi huo haukuwa na manufaa makubwa kwasababu bado timu hiyo ilikuwa ni kibonde katika ligi hadi kufikia kushuka daraja na kupotea katika anga ya soka kitaifa jambo lililodhihirisha wazi kuwa haikuwa na uwezo ila kinga yao kubwa ilikuwa ni waamuzi.

Lakini pia wakati Timu za Simba na Yanga zilipokuwa zinatumia Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam, kulikuwepo na taarifa na malalamiko kutoka kwa timu za mikoani kwamba wenyeweji walikuwa wanapendelewa na waamuzi.

Kwa hali hiyo inaonesha wazi kuwa 'mchezo mchafu' unaokuwa unalalamikiwa na timu hizi kuwa zinaumizwa na baadhi ya waamuzi umekuwa umeshamiri na kuota mizizi kwa miaka nenda rudi hivyo kazi ya kuing'o itakuwa ni ngumu na inayohitaji muda lakini si jambo la leo na kesho kisha kupata kitu kilicho bora.

Madhara yanayofanywa na baadhi ya waamuzi ndiyo kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya soka nchini ni ukweli usiopingika kwamba maendeleo bora ya soka yanategemeo mengi ikiwemo waamuzi walio bora na wenye uwezo wa kufanya maamuzi bila kuyumbishwa na mtu au kikundi fulani.

Licha ya kuwepo kwa waamuzi wenye uozo na wababaishaji wakubwa lakini ukweli ni kwamba wapo wengine walio safi na wenye mwelekeo wa kusimamia ukweli pasipo kuyumbishwa na mtu wala kundi fulani.
Waamuzi wa aina hii ni mfano wa kuigwa na kila mpenda kandanda nchini kwani wao ndiyo muarobaini wa kuendeleza soka la Tanzania.

Tunajua kwamba wapo baadhi ya waamuzi ambao ni safi wasiokuwa na shaka, wanaosimamia ukweli hadi mwisho. Hawa ndiyo wanaaotakiwa katika kuhakikisha kwamba wanafanya soka la Tanzania linakuwa na mwelekeo unaoeleweka kwa manuaa ya sasa na baadaye.

Kuna kila sababu ya kulipongeza Shirikisho la Soka nchini TFF kufuatia kuchuakua uamuzi mzito wa kuwafungia waamuzi kadhaa walioonekana kwamba ni kikwanzo katika maendeleo ya soka kwenye Taifa letu.

Hali hii ilikuwa ni moja ya njia ya kuhakikisha kwamba waamuzi wanaopewa dhamana ya kusimamia Ligi Kuu mwaka huu wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za soka.

TFF ilikuwa na kila sababu ya kusimamia ukweli huo kwa ajili ya kuinusuru hali ya soka la Tanzania lakini, hili si halitoshi pia kinachotakiwa ni kufanya usafi kwenye sekta ya waamuzi kwa mara nyingine ili kujisafuisha zaidi.

Huyu ndiye The Bossss pale Ikulu ya soka nchini Tanzania anaitwa Frederick Mwakalebela a.k.a Katibu Mkuu wa TFF.

Si hilo pekee lakini jambo lingine linalotakiwa kuangaliwa ni wenyewe TFF kama kuna baadhi ya vigogo wasiokuwa waamini ambao kwa namna moja amba nyingine wamekuwa wakishinikiza kwa timu fulani kuwa na matokeo ya anayotaka yeye ambalo si sahihi.

Itakuwa ni aibu kubwa kama shirikisho ambalo ndilo baba wa soka nchini, ikitokea kiongozi mmoja wa viongozi wa juu wa TFF, aanze kufanya hujuma za kupanga matokeo kwenye baadhi ya mechi ili aweze kunufaika kwa maslahi anayoyajua yeye.

Kinachotakiwa ni kwamba timu ziachwe ziamue zenyewe kulingana na uwezo wa timu husika. Kama timu uwezo wake ni mdogo basi zikubaliane na matokeo na zile zenye uwezo mkubwa ziachwe zipete. Mano mzuri tumeshuhudia vigogo wa soka la Bongo Simba na Yanga zikiwa zimelala ama kuambulia sare.

Haya ni matokeo yanayotoa changamoto kwa vigogo hao kwa kuwa wamekuwa hawaandai timu kwa kiwango kinachotakiwa bali wanakuwa wakijitutumua na kutumia mamiloni ya shilingi kununua wachezaji kutoka nje ya nchi ambao wengi wameshazeeka na wanashindwa kuendana na kasi ya wachezaji chipukizi waliopo katika baadhi ya timu.

Mambo haya ndiyo ambayo yanazikumba timu hizi kila mwaka kwa maana hazina utamaduni wa kuwa na kikosi kilichojengeka wa muda mrefu bali zinekuwa zikisajili wachezaji wapya kila mwaka hivyo kufanya walimu kuwa na kazi ya kusuka kikosi kipya kila mwaka.

Vile vile kwa upande wa benchi la ufundi la timu hizi limekuwa halidumu bali kila kukicha utakuta watu wanabadishwa na kuwekwa watu wapya huku wakifiri kwamba chanzo cha timu zao kufanya vibaya ni benchi la ufundi na kushindwa kuelewa dawa sahihi ya kuponya ugonjwa wao ilikuwa ni Panaldo na si Muarobaini kwani kinachotakiwa ni kuwa na kikosi cha muda mrefu.

Lazima kila mtu aelewe kwamba Tanzania inahitaji kuona timu zinashinda kulingana na uwezo wake na si kutegemea nguvu ya refa ili kuwa na bingwa mwene uwezo na si bora bingwa.

Tunataka bingwa mwenye uwezo wa kuwawakilisha vyemna watanzania zaidi ya milioni 34 ambao wengine wanazaliwa hadi wakati huu tunavyozunyumza. Vita ni ngumu lakini TFF tuliwakabidhi silaha za aina zote ili kuhakikisha kwamba tunaibuka washindi katika vita hii muhimu kwa nchi hetu, huo ndiyo moyo wa kizalendo unaotakiwa kufuatwa na kila Mtanzania na asiye Mtanzania.

HII NI EXCLUSIVE NEWS KUTOKA PALE MITAA YA Jangwani na Twiga almaarufu kama Yanga.

Mpoland kuinoa Yanga Kaunda

Wojciech Lazarek akiwa katika picha tofauti(picha kwa hisani ya mtandao wa Gooogle)

KOCHA mpya wa Yanga kutoka nchini Poland, Wojciech Lazarek, ataanza kuifundisha timu hiyo katika Uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya Klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo ambazo zilidhibitishwa na mmoja wa viongozi wa juu wa Yanga, zilisema kwamba Lazarek huenda akautumia Uwanja huo baada ya ukarabati wake kukamilika kwa asilimia 40.

Kiongozi huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema juhudi za makusudi zinafanyika ili kuhakikisha ujenzi wa Uwanja wa Kaunda unakwenda haraka ili Lazarek akitua aukute ukiwa tayari ama katika hatua za mwisho.

"Kama mlivyotangaziwa kwamba Kocha Lazarek, atatua mapema Oktoba 12, mwaka huu na baada ya kumalizana naye atarejea nchini kwao kwa ajili ya kuchukua vifaa vyake na baadaye kurejea kuinoa Yanga.

"Wakati huo sisi tutajitahidi uwanja wetu uishe mapema ili timu iwe inafundishwa hapa hapa lengo likiwa kumwezesha kocha wetu kufanya kazi kirahisi lakini kubwa kuliko yote ni kupunguza matumizi kwa kulipia viwanja vya nje ya klabu," alisema Kiongozi huyo.

Kocha Lazarek (69) alitangazwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega, kuwa ndiye atakayechukua nafasi ya Mserbia Milutin Sredojevic 'Micho'(37) ambaye alibwaga manyanga mara baada ya Ligi Ndogo ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kumalizika.

Naye Mweka hazina wa klabu hiyo, Abeid Abeid 'Falcon' alisema kuwa suala la ujenzi huo linakwenda vizuri kama lilivyopangwa na hivi sasa wapo katika hatua ya tatu ambayo ni kuweka mchanga maalum kwa ajili ya kuzuia magugu kuota.

Falcon aliongeza kuwa mbegu za kupandwa uwanjani hapo zinatarajia kuwasili wakati wowote kuanzia sasa zikitokea nchini Afrika Kusini, baada ya shughuli za awali kukamilika na kwamba zitaoteshwa kwa siku 20 tu.

Yanga mishoni mwa wiki iliyopita ilishinda ikiwa ni mchezo wa pili tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera. Matokeo hayo yanakuja ikiwa ni siku chache tangu Uongozi kuunda kamati ya ushindi iliyowahusisha Francis Kifukwe, Baraka Igangula na Jamal Malizi waliokuwa viongozi wa zamani wa klabu hiyo kubwa nchini.

Thursday, October 4, 2007

HAYA NDIYO MAISHA YA MASTAA WA MAMTONI

Mtangazaji Redio One atembea uchi mtaani
London, Uingereza

KATIKA harakati za kupinga kutukanwa na wasikilizaji wake, mtangazaji na Dj maarufu wa kituo cha Redio One cha nchini Uingereza, Edith Bowman ametembea uchi mitaani.

Gazeti la The Sun la nchini humo katikati ya wiki liliandika kuwa mtangazaji huyo aliamua kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili za msingi, ambazo ni kupinga kutukanwa na wasikilizaji wake na kutoa shukurani baada ya mama yake mzazi kupata nafuu ya matatizo ya Saratani ya matiti.

Marafiki wa karibu na Edith ambao ni Alicia na Dita hawakufurahishwa na kitendo hicho hivyo walichukua jukumu la kumkamata na kumvisha nguo ili kumsetiri na aibu hiyo.

Alipoulizwa juu ya suala hilo, Edith alisema, "nimechoka kutukanwa kila wakati na watu wasiokuwa na shukurani kwa kile ninachokifanya lakini lingine lililonifurahisha ni kitendo cha mama yangu kupata nafuu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya Saratani kwa muda mrefu".

Edith wa mtangazaji wa Radio one ya nchini Uingereza

=======================================

Ulokole wamshinda Bertha BBA

Pritoria, Afrika Kusini

MSHIRIKI wa shindano la Big Brother Afrika (BBA), kutoka nchini Zimbabwe, Bertha ameshindwa kuilinda imani yake ya kilokole baada ya kuonekana akiendelea kuogelea katika mahaba na mpenzi wake wa Ghana, Kwaku.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mzimbabwe huyo alitangaza kuachana na mambo yote maovu ikiwa ni pamoja na kumtema mpenziye Kwaku.

Mwanadada huyo alisema lengo lake ni kutaka kuwa mfano bora kwa washiriki wengine katika jumba hilo, lakini hata hivyo, ameshindwa kuzishinda tamaa za mwili.

Kamera zilizotanda katika jumba hilo, jana zilithibitisha kuwa Bertha ameshindwa kwenda sambamba na imani ya kilokole baada ya kumuonesha akiwa anaendelea kuponda raha na Mghana huyo.

Kama vile haitoshi Bertha ameendelea kufanya vituko kama kubadilisha nguo akiwa na Kwaku jambo amablo ni kinyume na imani ya dini aliyotangaza kujiunga nayo.

Kama hujawahi kuangalia shindano la Big Brother Africa basi, elewa kwamba huyu ndiye Bertha moja ya washiriki wa shindani hilo kubwa barani Afrika.
=======================================

Pamela Anderson kufunga ndoa ya tatu

Las Vegas, Marekani

MSANII Pamela Anderson, amesema wakati wowote kuanzia sasa anatarajia kuingia kwa mara ya tatu katika maisha ya ndoa takatifu.

Pamela (40) maarufu kama Pammi aliwaambia waandishi wa habari nchini humo kuwa tayari serikali ya jimbo la Las Vegas imempatia leseni ya kufunga ndoa na mpenzi wake aitwaye, Rick Salomon.

Salomon (39) ambaye ni mchezaji mahiri wa mchezo wa Poker alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri katika filamu ya msanii, Paris Hilton iitwayo 'Couple', iliyochezwa miaka minne iliyopita.

"Wakati wa kuteseka na kuficha penzi letu mbele ya umma umekwisha, kwa hiyo nimeamua kwa moyo mweupe Pammi awe mke wangu wa maisha," alisema Salomon.

Pamela ameshaolewa mara mbili na kuachika hivyo endapo atafanikiwa kufunga ndoa na Salomon, hiyo itakuwa ndoa yake ya tatu.

Hizi ni baadhi ya picha za msanii wa Pamela Anderson akiwa katika mapozi tofauti. shukrani kwa mtandao wa Google kwa kufanikisha upatikanaji wa oicha hizi muhimu.

============================================================

Eva aanika ngono kwenye mtandao

Califonia, Marekani

MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini Marekani, Eva Longoria anadaiwa kucheza filamu ya ngono na kuianika kwenye mtandao wa Internet.

Filamu hiyo ambayo alishirikiana na baadhi ya nguli wa mpira wa kikapu wanaoshiriki Ligi Kuu ya mchezo huo nchini humo maarufu kama NBA, inalaaniwa vikali na wakazi wa nchini Marekani.

Mchezaji Tony Parker ni mmoja wa washiriki wa filamu hiyo ambayo imesambazwa kwenye mtandao wa Internet.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba chanzo cha Longoria kuanika uchafu huo kwenye mtandao ilikuwa ni ili kupata maoni juu ya mwenendo wa filamu hiyo iitwayo 'The reality of life' ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuiingiza sokoni.

Huyu ndiye Eva Longoria

Huo ndio uhondo wa mastaa wa majuu mastaa wa Bongo vipi mnaubavu wa kufanya haya? kazi kwenu lakini eleweni kuwa mila na desturi zetu hazifanani kamwe.

=======================================